[7/6/2015, 06:17] Sara Dadi: Asalaam alaykum warahmatullah wabarakatuh. Vipi hali zenu ndugu zangu?
[7/6/2015, 06:19] Sara Dadi:
??HAMASAAT?
?
⏩Miinamo yote inavunja mgongo!!
ila miinamo ya "swala" kwayo roho inatukuka na kuinuka
⏩Misikiti ni madrasa ambayo watoto wetu wanajifunza qur-an na adabu.. usimkoseshe mtoto wako kheri hii na usiwakoseshe watoto wengine kwa mikaripo mikali wanapokosea bali huruma na upole ndiyo malezi
⏩Hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya bali sema hiyo ni kheri yangu na muachie mambo yako Mwenyezi Mungu
⏩Daima inayoleta nuksi si bahati (mbaya)
bali madhambi yaliyosongamana na ambayo mengi yao tushayasahau [hakika maasi yanaondoa neema]
⏩Pale unapofanyiwa maudhi usifikirie kurudishia kwa "nguvu" bali fikiria kurudishia kwa "uzuri"
{Na wema na ubaya hauwi sawa, peleka lililo bora}
⏩Laiti wanawake wangejua..
kwamba Mwenyezi Mungu anawazidishia uzuri mbele ya macho ya wanaume..
kila ambapo anayejisitiri miongoni mwao anazidi kujisitiri kuliko anayejianika
⏩Watu wananunua vitu wasivyovihitaji, kwa pesa wasiyokuwa nayo, ili wajionyeshe kwa watu wasiowapenda
⏩Vuta pumzi na lijaze pafu lako hewa.. na sema "alhamdulillah mimi nina hali nzuri"
na jiridhishe kwamba leo ni bora kuliko jana, na kesho kwa idhini ya Mola itakuwa nzuri zadi
⏩Hakuna anayekuzuia kutabasamu na hakuna kitu kinachostahiki huzuni.. maisha yanageuka na wewe unatakiwa ukinaike kwamba yaliyopita yashakufa na yajayo yashaandikwa
⏩Siku mpya kwenye mwezi wa fadhila, kwa tabasamu, matumaini, na dua.. ewe Mola panda kwenye nyoyo zetu raha na zijaze matumaini yasiyokatika daima..
⏩Ewe Mola wape shifaa wagonjwa wetu na wagonjwa waislamu na warehemu maiti wetu na maiti waislamu;
ewe Mola hakika sisi tuna wapendwa waliofariki dunia; ewe Mola tukutanishe pamoja kwenye pepo yenye neema.
Ewe Mola zihifadhi nchi zetu na zihifadhi nchi za kiislamu na waislamu.
Ewe Mola tupe amani kwenye watani zetu.
Ewe Mola tuhifadhi na fitina za siri na za dhahiri
?TUAMRISHANE?
?MEMA?
Imeletwa kwenu na Sara Dadi